1.UKOSEFU WA MAARIFA SAHIHI
-Ni vizuri ikafahamika kuwa kilimo ni utaalamu kabisa (Sayansi) kama ilivyo udaktari au uhandisi au fani yoyote ile inayohitaji maarifa.Ndio maana mimea usipojua mahitaji yake kwa wakati sahihi, baadhi itakufa, au itakuletea mavuno hafifu, n,k
Hivyo kabla ya kwenda shambani na kuwekeza muda wako na pesa zako, ni muhimu sana KWANZA ukajifunza kupata maarifa sahihi ya kitu gani unataka kuzalisha, mbegu gani utatumia, madawa (WADUDU &UKUNGU), mbolea, wadudu gani waharibfu utakabiliana nao vipi, utahifadhi vipi mazao yako baada ya kuvuna na mambo mengine mengi.
BILA KUFANYA HIVYO UTAPATA HASARA TU, kwa sababu sasa hivi kilimo ni soko huria, hivyo utakutana na pembejeo feki nyingi sana za kilimo humo madukani, wauzaji na wasambazaji BAADHI SI WAAMINIFU (ANZIA MBEGU, MADAWA, MBOLEA).
Utapanda mbegu feki hazitaota, utatumia madawa feki yata kuunguzia mimea yako, na wakati mwingine utauziwa madawa hata iaina 5 yanayofanya kazi mmoja ya kuua wadudu (hivyo kupoteza fedha zako). Ukisosa maarifa sahihi utakuwa mtu wa kutanga tanga tu, kwa mfano wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia wewe unaweka mbolea ya kupandia, wakati yan kuweka dawa za kukinga mimea yako na ukungu wewe unaweka dawa za kuua wadudu, aina fulani ya dawa hazifai kuua magugu ukiwa umeshapanda mimea wewe utatumia tu kiua gugu chochote herbicides bila kujua ipi inafaa wakati gani, hivyo utapoteza pesa zako nyingi kwa kutanga tanga na kutokujua ufanye nini kwa wakati sahihi
-Jambo lingine sambamba na maarifa, ni kuwa UNAPASWA KUANZIA SOKONI KWANZA KABLA YA KUZALISHA ZAO LOLOTE LILE, LENGO NI UJUE
i). NI ZAO GANI LINAKUWA ADIMU/LINAPENDWA SOKONI (WALAJI) WAKATI GANI LINAKUWEPO SOKONI KWA WINGI AU LINAKUWA NA MAHITAJI MAKUBWA-
Lengo la kutambua hili ni Ili sasa ukajipange kuzalisha kuendana na mahitaji ya soko, ili huo wakati uatao vuna na kupeleka sokoni ukutane na bei nzuri kwa maana ya demand and supply-kama mzigo upo kidogo sokoni na mahitaji ni makubwa automatically bei itakuwa juu na hivyo kuwa faida kwako wewe mzalishaji.
Mfano kwa uzoefu wangu- nafahamu mazao mengi sana huwa adimu sokoni kuanzia miezi ya disemba hadi April maana mvua huwa nyingi nyakati hizo hivyo wengi huogopa kuzalisha wakati huo kuhofia mafuriko, wadudu na magonjwa ya ukungu ni mengi sana, na hapo ndio bei za vyakula huwa juu, hivyo ukiweza kutime nyakati hizo lazima utapata faida
ii). NI MUHIMU PIA KUTAFITI, ni aina ipi ya hilo zao linapendwa sana na walaji, mfano je walaji wanapenda nyanya size nene sana, au saizi ya kati au ndogondogo, au mfano katika matikiti je wanapenda ya rangi zenye michirizi maarufu kama zebra, au ya kawada, je katika Karoti wanapenda karoti fupi nene, au nyembamba ndefu, au mfano katika kabichi walaji/soko wanapenda za iana gani zenye ngozi ngumu na umbo kubwa (kilo 4-7 etc) au saizi ndogo? etc.
2. UKOSEFU WA MAANDALIZI SAHIHI (MTAJI)
Wakulima wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawakujipanga, kuanisha mahitaji mahususi yanayotakiwa katika kilimo husika, hawakujipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mfano- (Mkulima hakupiga mahesabu sahihi ya mahitaji ya shamba lake tangu kuandaa shamba, kupanda, mbegu madawa, mbolea, palizi, mavuno, hadi kufikisha sokoni) anapoanza kilimo akikutana na changamoto mfano za mbolea za kupandia, kukuzia, au za maua na matunda (booster), pesa inakata naye anakata tamaa anaamua kuzalisha tu ili mradi au kutelekeza mashamba, hivyo ni muhimu sana , kujipanga kabla ya kuanza shughuli yoyote, ambayo utajitoa muda wako na pesa yako.
Wasalaamu.
mawasiliano. kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxx